Psalms 45:1-6

Wimbo Wa Arusi Ya Kifalme

(Kwa Mwimbishaji: Utenzi Wa Wana Wa Kora)


1 Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema
ninapomsimulia mfalme mabeti yangu;
ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi.


2 aWewe ni bora kuliko watu wengine wote
na midomo yako imepakwa neema,
kwa kuwa Mungu amekubariki milele.

3 bJifunge upanga wako pajani mwako, ee mwenye nguvu,
jivike fahari na utukufu.

4 cKatika fahari yako, songa mbele kwa ushindi,
kwa ajili ya kweli, unyenyekevu na haki,
mkono wako wa kuume na uonyeshe matendo ya kutisha.

5 dMishale yako mikali na ichome mioyo ya adui za mfalme,
mataifa na yaanguke chini ya nyayo zako.

6 eEe Mungu, kiti chako cha enzi
kitadumu milele na milele,
fimbo ya utawala wa haki
itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako.
Copyright information for SwhKC